Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, January 22, 2006
UCHUNGU KATIKA NCHI YANGU!!!


Good Samaritans trying to rush to hospital a pedestrian who was shot by four robbers suspected to be involved in a robbery that occurred at Eljabri Jewelers shop at Mkunguni/Livingston Streets, Kariakoo, Dar es Salaam on Saturday. Tsh. 300,000, a gun and other property were stolen. Although the bandits were reported killed by the police on the same evening, there is confused information about whether the killed persons were robbers or not . (Photo by Peter Mgongo).
 
© boniphace Tarehe 1/22/2006 01:56:00 PM | Permalink |


Comments: 8


 • Tarehe 1/23/2006 10:07 PM, Mtoa Maoni: Blogger nyembo

  Vipi umeshindwa kutafsiri Lugha hiyo ya kigeni ili isomeke katika Lugha ya kiswahili na kwa nini hukutuomba radhi wasomaji wako tuondokane na tegemeo letu kuwa tutasoma jambo kwa KISWAHILI badala yake tukakuta tutasoma Lugha hiyo ya Wakoloni?
  jaribu kututhamini zaidi sisi tupendao kupitia katika blog yako haswa kwa furaha ya matumizi ya Lugha adhimu ya Kiswahili

   
 • Tarehe 1/24/2006 4:13 AM, Mtoa Maoni: Blogger mloyi

  majambazi motoPolisi wanajiuliza hao majambazi wamepata wapi moto huo? nao wameiga. Simama kama hutaki risasi! wengine wanasema Wao wanakamata na kuhukumu wenyewe. Fikiria ukikamatwa na kesi ya ujambazi, ambayo adhabu yake ni miaka 30 jela!, halafu polisi aliyekukamata anakupa mia tano kwa heshima anakuomba ukamnunulie sigara mtaa wa pili! utadhani ni dhali la mentali ujaribu bahati yako kukimbia huo ndio utakuwa mwisho wako huko mbele wameshajipanga na mabunduki yao , jaribu uyapechakula. Siku hizi wajanja wakipewa bahati hiyo wanakataa katakata!

   
 • Tarehe 1/24/2006 9:46 AM, Mtoa Maoni: Blogger Boniphace Makene

  Kumradhi kwako Nyembo na wengine. Nilikuwa nakimbia nikakutana na habari hiyo katika gazeti la The Express nikaona nisiichafue na kufuta umiliki wake. Kosa langu sikuomba radhi kwa usumbufu niliowasababishia lakini ada ya mja unena muungwana ni vitendo. Naomba radhi kwa tukio hili.

   
 • Tarehe 1/24/2006 12:24 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

  Bonny, hakika kwa mtindo huu bongo kunatisha kurejea. Umesikia ile ya askari polisi kuwatwangilia mbali visogoni raia wasio na hatia na kuwaacha majambazi husika. Sasa hali halisi ni kutarajia kutwangwa risasi wakati wowote ama na polisi ama na majambazi, kwa kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya.

   
 • Tarehe 1/24/2006 4:31 PM, Mtoa Maoni: Blogger Boniphace Makene

  Kaka bado akina hawa wanaojifanya kubandika makala za kuchoma katika makasri, mabaragumu, majikomboe, maharakati, manuru akilini, mamwandani nk wakijulikana tu wajiandalie makabuli maana sasa rahisi sana kuwatia mauti kwa kisingizio cha ujambazi. Tena ndugu yangu Mwaipopo usijisumbue kununua gari maana hilo ndilo litatumika kukubeba kukupeleka mazikoni. Jamani tena hakuna wa kuweza kutuhepusha na balaa hili. Sijui ngoja nifikiri upya...

   
 • Tarehe 1/25/2006 3:26 AM, Mtoa Maoni: Blogger nyembo

  hakuna uoga kwa wakati ujao, naona wazi kuwa wanamakasri na wengine tunapata changamoto hapo!

   
 • Tarehe 1/25/2006 6:47 AM, Mtoa Maoni: Blogger Fikrathabiti

  Kikwete ameunda tume ya uchunguzi. sasa asije akala matapishi yake mwenyewe!!!Wakati akihutubia bunge aliweka wazi kua kuna ulazima wa kuzitoa taarifa za tume za uchunguzi hadharani ili waungwane waweze kujua kinagaubaga wa uzembe na uozo uliopo katika utendaji wa kazi wa vyombo vya dola.

  Hii kwake ni changamoto kwahiyo tusubiri kwa mara ya kwanza kuona vigogo wakiadhibiwa kwa uzembe ulio wazi baada ya kuvumiliwa kwa mda mrefu!!

   
 • Tarehe 1/29/2006 10:52 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Ujambazi, risasi, damu, vifo na mengine yanayoendana na kasi hii ya vijana wanaotaka nao kufaidi keki ya nchi ni sehemu tu ya vielelezo vya kitu Boniphace kaita, "kupanuka kwa wigo wa walio nacho na wasionacho." Sasa wawekezaji wanataka kuanza kuwekeza kwenye magereza kama ilivyo nchi mbalimbali duniani. Gereza linamilikiwa na kampuni binafsi. Hivyo ili hiyo kampuni ipate faida, inapaswa kupata wafungwa wengi. Hivyo uhalifu unakuwa ni aina ya kitega uchumi.

  Mbona bado hatujaona mambo?

  Hili la tume...Tanzania kwa tume naivulia kofia. Lakini matokeo ya hizi tume ni nini hasa? Tume hutufanya tuamini kuwa tatizo linashughulikiwa. Kumbuka Mkapa alivyokuja kwa mbio za tume ya rushwa...rushwa ndio ikaongezeka ikaingia hadi ikulu kwake.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved