Rabuka Mola jalia, mwanao kuamkani
Shairi pate tungia, Bloguni somekani
Ahadi nilitolea, hima vema timizani
Ripoti kuandikia, ya mwezi uloishani.
Kazi tulojipatia, njema wewe wasifuni
Watu tunawafunzia, maarifa ongezani
Pamoja twakatalia, maovu kufanyikani
Mola Baba angazia, taifa la bloguni.
Mwezi ulioishia, chache zilianzishwani
MAISHA TAFAKARIA, Musoma ikatokani
KURUNZI kamulikia, kutokea mabondeni
Alabama kasikia, Sauti
BARAGUMUNI.
Wito sijasahulia, weledi jitambueni
Tafakari nafanyia,
Blogu KiswahiliniHoja mlizotolea, ndizo naunganishani
Kisha wote kuonea, kile mchokifanyani.
Pale nilipoishia, Kanada nikaendani
Harakati kakutia, Toronto kusalimuni
Ilikuwa yavutia, gwiji huyu muonani
Ndesanjo kakumbukia, simu kutupigiani.
Sasa wazi naanzia, wote sasa tuliani
KASRI niliishia, siasa shabikiani
MATERU bila julia, naye moto kawashani
Ukweli katupashia, Zanzibar iko motoni.
Hoja ya kuweka picha,
JIKOMBOE katoani
Riwaya kushikilia,
HARAKATI jikitani
BWAYA yeye katania, nani anayesomani
Majibu akapatia, hoja yake ifutani.
Hotuba ilo sawia, igizo jipya nchini
Blogu zikasemea, lazima kuitunzani
MARK kaitafutia, JEFF kaitundikani
Lengo kuja tazamia, Kikweto alofanyani!
DAMIJA kaendelea, Blogu jina pewani
Wasifu kiandikia, lini wangu tatoani
MWANDANI alopotea, kaleta hoja razini
Katwambia kumbukia, nyumbani bora nchini!
Huko Dodoma nalia, sijui chawakinzani
MIRUKO alikimbia, Polisi tukasemani
MARTHA naye kaamua, kwa mwezi kuja mojani
Simanzi kanachilia, kushindwa kumsomani.
Hawa sasa nasemea, kweli wamekimbiani
FATMA mwanasheria, London kajifichani
NGURUMO wa Tanzania, kajificha gazetini
Kila anapotokea, semina kitangazani!
KAKA PORI katokea, tathimini angazani
Teknojia yakua, hata huko maporini
Sasa anaandikia, na picha kisha wekani
NYEMBO kamkumbushia, ya Kikwete kuhojini.
Bibie
CHEMI nasema, hongera mama semani
Urembo wanafanyia, wanitia walakini
MOTOWAKA nakwambia, picha yako iwekeni
Maana utajulia,
KESSY ukimuonani.
Ewe
MKWINDA julia, kaziyo twaheshimuni
Tazama wageuzia, wengi ngano kutungani
MKINA mpe gunia, arejeee duniani
PAMBAZUKO tambulia, wajibu kuandikani.
ZAINABU na
BAKANJA, hawa ni wa msimuni
BITIDAFFA wa Dodoma, naye amejiungani
KAZONTA anafatia, mgomo kuendeshani
Watwacha kwenye udhia, sisi kutowasomani!
Mwisho wake
BANGAIZA, mimi sijaufikani
TERRIE wewe nakwambia, subiri nakufatani
KIVALE namuonea, kimya kakumbatiani
Naomba jibu patiwa, yupi hawa amshani?
Hoja uliyotolea,
MSANGI toka nyandani
Hima wazi jadilia, kwani ina utatani
Tumeshaanza onea, madaraka jipeani
Huu utata anzia, wa wanamtandaoni.
MICHUZI sijachelea, picha zako kusifuni
Bongo unaangazia, ughaibuni onani
Nasi sasa twaigia, bila woga anikani
Kumbuka wito natoa, kwa wengine kupitani.
Umoja wetu jalia, twapaswa kuukuzani
Nguvu tukizingatia, wengi itawawashani
Kumbuka ni yetu nia, mpya nyingi funguani
Macho wakishafumbua, Tanzania tachekani.
GAPHIZ unosomea, nawe nakukumbukani
Mwaka mpya kutokea, Heri ukatupeani
Nami sasa nasemea, kazi njema tufanyeni
Vitabu tukifunua, hazina tutapatani.
Kaditama naishia, Texas kuishini
Wito niliutolea, Mellisa kikubalini
Kwangu amenitokea, fikira kufufuani
Simba naweza vamia, bila woga nipatani.
Ahsante Makene,
Leo sijui hata kichwa changu kinaongea lugha gani.Maisha ya ughaibuni lah,kama mnavyojua.Lakini baada ya kusoma ripoti kama hii basi tabasamu linajongea.Ahsante Makene