Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, January 29, 2006
NINI VYANZO VYA AJALI TANZANIA?

Sarah Daudi Mfanyabiashara wa Dar es Salaam (Kulia) akiugulia kwa maumivu kufuatia ajali ya lori lenye namba za usajili T 181 AGT alilokuwa akisafiria kupinduka kulikotokana na tairi moja la upande wa kushoto kupasuka. Lori hilo lilikuwa likitoka Lushoto kuelekea Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na ajali hii ilitokea eneo la Maili Tano. Dereva wa Lori hilo ambaye aliumia vibaya alitambuliwa kwa jina moja la Jang'andu. (Picha na Peter Mgongo). (Nimetafsiri hili kwa heshima ya wasomaji wangu wa Kiswahili)

NIMEKAA kipindi kirefu kuangalia vyanzo vya ajali Tanzania. Kwa taarifa yako ajali ni moja ya vyanzo vikubwa vya maafa katika Tanzania inayofatana kabisa na idadi ya wanaokufa kwa malaria na kisha magonjwa kama ukimwi hufuatia.

Katika kufikiri nikagundua haya, kukosekana sheria za kudhibiti leseni za kuendeshea magari, kutokaguliwa magari yanayoendeshwa, kutokuwa na sheria ya kubana unywaji pombe wakati na kabla ya kuendesha na pia kukithiri kwa rushwa katika makosa yanayoambatana na matumizi yasopasa ya barabara. Nchini Tanzania mtembea kwa miguu hana haki ya kutumia barabara na mwenye gari ni Mungu. Leseni za kuendesha utolewa kwa dakika tu bila kupima viwango vya dereva. Kutokana na hilo madereva wengi hawana uwezo wa kuepa ajali na hivyo kama hakutakuwa na mkakati wa kudhibiti leseni za madereva, kukagua magari yanayosafiri basi ajali zitazidi kuongezeka. Hoja hii imekuja baada ya kukuta picha hii katika gazeti la The Express linalohaririwa na rafiki yangu Fatma Bapumia.(Huyu nilisoma naye Chuo cha Uandishi wa Habari TSJ na kisha tukawa wote Chuo Kikuu Dar es Salaam)
 
© boniphace Tarehe 1/29/2006 11:27:00 AM | Permalink |


Comments: 3


  • Tarehe 1/29/2006 6:27 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Vyanzo vya ajali ulivyoviweka bayana hapa ni kweli kabisa.Labda tuanze kujiuliza,mpaka lini??/

     
  • Tarehe 2/02/2006 2:38 AM, Mtoa Maoni: Blogger FOSEWERD Initiatives

    na hushughulikiwa kwa zima moto style.....watu wakisahau wao wanaacha....namuonea huruma huyo mama nimejiweka kwenye nafasi yake!!

     
  • Tarehe 4/21/2007 9:34 AM, Mtoa Maoni: Blogger Mikundu Matako Makalio Manundu

    Ahsante sana kwa kutafsiri, imetusaidia sisi, sasa nakutakeni mpitie kwa Mzee wa Mikundu, kujiliwaza kidogo na picha za makalio, nyeto ruksa:
    http://mikundu.blogspot.com/

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved