Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, January 19, 2006
MIFUKO YA PLASTIKI TANZANIA ITAIGA LINI RWANDA?
KATIKA vitu vinavyochangia uharibifu wa mazingira ni mifuko ya Plastiki. Mifuko hii licha ya madhara yake kwa binadamu imekuwa ikipingwa vita ya chini chini hapo Tanzania. Hakuna jitihada za dhati za kuiondosha. Sasa hivi tunapokumbwa na ukame na majanga kama njaa tunashindwa kukumbuka kuwa ardhi inapofunikwa na mifuko ya plastiki pia huathiri uoto wake. Soma hapa kuona harakati za Rwanda katika kupambana na mifuko hiyo huko.
 
© boniphace Tarehe 1/19/2006 12:52:00 PM | Permalink |


Comments: 3


 • Tarehe 1/20/2006 5:36 PM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Makene na wewe mbona unakosea? Hiyo sio mifuko ya plastiki. Inaitwa Rambo!

   
 • Tarehe 1/21/2006 10:57 AM, Mtoa Maoni: Blogger Boniphace Makene

  Ndesanjo nilisahau hilo jina

   
 • Tarehe 1/21/2006 2:33 PM, Mtoa Maoni: Anonymous mwaipopo

  Kule Arusha inaitwa Malboro. Watu wa Arusha nao wana Kiswahili chao Ukisema Rambo hawakuelewi, Ukisema 'ndala' hawakuelewi mpaka useme 'malapa'.

  Salamu ya vijana wengi kule Arusha sio 'mambo' ni 'niaje'

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved