Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, January 29, 2006
KUHUSU HATI YA MUUNGANO: MWANASHERIA ZANZIBAR AJICHANGANYA
KAMA ilivyo kawaida ya viongozi wa Tanzania kutokutunza kumbukumbu au kujifanya wako juu ya wengine, ndivyo inavyojionyesha katika habari hii. Hati za Muungano ziliwahi kutamkwa na Mwanasheria huyo kuwa hazipo katika ofisi yake lakini sasa anapoona mambo yanazidi kutanuka anaingia na hoja ya kisiasa isiyoendana kabisa na majukumu ya kazi yake ambayo kwa dhati hayausihani na kutetea upande wowote zaidi ya kutazama mhimili wa sheria. Kutunza matatizo si kuyatatua na kama Zanzibar wanadhani kuwa wakimya katika masuala ya Muungano ni kuunufaisha Muungano wanakosea. Masuala ya Muungano yana haki ya kujadiliwa na kuzungumzwa na yeyote maana athari za Muungano si za kundi moja.

Msimamamo wa Kasri la Mwanazuo katika hoja ya Muungano ni mmoja. Hati ziwekwe wazi na jamii ijadili. Kasri linahitaji kuona Muungano wa Afrika na kuwa taifa lakini linasisitiza juu ya hatua zote kufanyika kwa uwazi, kufutwa kwa hoja za siri na pia kuwepo tashwishi la kufikia maafikiano na Muungano ili waafrika waambae katika Bara lao bila mipaka. Kuungana kwa Afrika hakuna maana kuwa aina nyingine za kuungana kama kwa Tanganyika na Zanzibar kunyamazishwe bila kutafuta mbinu za kuunganisha za kisayansi kama alivyowahi kudokeza Fredrick Taylor.
 
© boniphace Tarehe 1/29/2006 11:01:00 AM | Permalink |


Comments: 2


 • Tarehe 1/29/2006 5:37 PM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Makene, hivi huyu mwanasheria ana nini? Kwani wakitokea watu wakiwa na ajenda ya kisiasa ni kosa? Kuwa na ajenda ya kisiasa ni kinyume cha sheria gani? Sikujua kuwa kuwa na hairuhusiwi kwa raia kuwa na ajenda ya kisiasa. Wawe na ajenda ya kisiasa au kisiase au kisiaso...wana haki ya kuuliza hati za muungano ziko wapi. Tena sio lazima wawakilishe wazanzibari wote. Wanawakilisha uraia wao. Hebu waache kuleta za kuleta.

   
 • Tarehe 2/02/2006 2:42 AM, Mtoa Maoni: Blogger mark msaki

  kasri, katika hili tunasimama wote. na ndio baadhi ya yale mazingaombwe ya mwalimu yanayotuumiza kichw kila kukicha..wazanzibari hawa si watu wa mwanzo kudai marekebisho / uhalali wa muungano. kujua uhalali wake ni jambo la kwanza kabla ya kufanya marekebisho. nakumbuka G 55 pia walidai, mwalimu akawazaba cha usoni...wengi waliteseka sana baada ya hapo kutokana na msimamo wao...jana G 10 wamerudi tena wanasema sasa watapeleka suala hilo mahakama ya dunia....

  tuko wote, kwangu mimi ni hatua ya mwanzo katika juhudi ya kuongoza jamhuri ya watu wa tanzania na sio jamhuri ya mawe ya tanzania!

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved