Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, January 12, 2006
HAMKANI SAFARI YAENDELEA KWA KASI, MBUROGU MPYA HIYOOO!
NATUMIA jina Mburogu kutoka kwa mtani wangu mmoja wa Kenya lakini haina maana kuwa nimelihalalisha! Lakini sasa ile kasi ya kuongeza Watanzania katika teknolojia hii inazidi kuchukua picha na hapa ninamtangaza kwenu NDYEMALILA anayeblogu toka Arusha. Mtembeleeni kama ilivyo ada na kumsabahi. Wakati ninapomtangaza huyu nazidi kutoa rai ya waheshimiwa wanablogu kuongeza jitihada ya kusaka wavunaji maana wasomaji ni wengi lakini wanablogu ni wachache.
 
© boniphace Tarehe 1/12/2006 07:28:00 AM | Permalink |


Comments: 1


 • Tarehe 1/16/2006 1:47 AM, Mtoa Maoni: Blogger Bwaya

  Makene nimesoma makala yako kwenye Mwananchi kuhusu nafasi ya Wabongo walio nje ya nchi. Makala hiyo imetulia.
  Mimi naomba nichangie kidogo kwenye swali lako lililohoji umuhimu wakujaza wanafunzi kwenye kozi kama PSPA, Sociology n.k wakati nchi ikihitaji walimu.
  Hili huwa najiuliza (si mara moja) kutokana na kilio cha Serikali kwamba inahitaji walimu. Kinachonishangaza mimi ni mbinu zinazotumika kuwapata walimu hao.
  Tungetegemea ongezeko mara dufu la wanafunzi walimu katika kitivo cha elimu (na labda) vyuo vya elimu vinavyotoa stashahada.
  Ajabu ni kwamba sasa hivi kinachofanyika ni kufupisha muda wa kozi na hata kupata walimu kwa mtindo wa rasha rasha ya semina ya wiki mbili!
  Nafikiri Serikali ilipaswa kufikiri zaidi katika hili. Ingeweza hata kuwaongezea wanafunzi wa vitivo vingine kozi ya elimu ili waweze kufundisha wanaposubiri kuajiriwa katika fani zao.
  Niliwahi kusoma ripoti moja kuwa elimu ya Tanzania inadidimizwa. Pamoja na sababu nyingine, ulipuaji katika kuwaivisha walimu, ulitajwa! Lakini naogopa kuunga mkono ripoti hiyo maana serikali ikisikia patakuwa hapatoshi! (Rejea HakiElimu)
  Uliseam kitu cha maana nashauri ukiandalie makala kamili kuaqnzisha mjadala.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved