Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, January 26, 2006
GAZETI TANDO JIPYA LATANGAZA HATARI TANZANIA
Kama kulewa madaraka, sijui kutafuta namna za kulejesha fedha walizotumia kugawa rushwa ama nini sijui? Haya yametokea na yameanza mapema sana baada ya wanasiasa wa Tanzania katika kipindi hiki ambapo nchi inakabiliwa na janga la njaa, ujambazi ambao hasa unatokana na kutanuka kwa wigo wa walio nacho na wasio nacho, kupanuka kwa matumizi ya serikali n.k, basi kama haitoshi viongozi wapya wanatangaza kutaka kuongezewa mishahara na marupururupu kibao. Hii inatia huruma namna walivyo vipofu hawa, inatia hasira namna wasivyotambua wanaowawakilisha, inaumiza moyo kuna wamesahau sasa hivi tu au ni ulimbukeni kama nilivyowahi kubainisha kwa JEFF pale Toronto. Hivi gari la Milioni 50 na hoteli za kifahari na mavazi ya mbwembwe yanayotengenezwa Marekani na Uingereza ndio Ubunge?

Nisichafue radha ya kumkaribisha Ndugu Mustapha anayekuja kwa kali hiyo na Gazeti Tando lake liitwalo Hotspot. Karibu Mustapha nadhani utashangaa jamii hii inayomiliki Magazeti Tando ilivyo na ukarimu kwa namna itakavyopita kwako leo hii hii kukukaribisha.

Kwa taarifa tu, Blogu hii imefunguliwa na Mustapha jana usiku baada ya mazungumzo yangu na January John akiwa Illinois kwa simu huku yeye January akichati na Mustapha kupitia kisemeo cha Yahoo. Hii kasi inanipa faraja sana kisa cha kuweka kando mjadala wangu na Nyembo kama ulivyoongezwa pia na MKWINDA. Nitarejea kwa hawa baadaye.
 
© boniphace Tarehe 1/26/2006 08:20:00 AM | Permalink |


Comments: 3


 • Tarehe 1/26/2006 9:11 AM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

  Karibu mwanakwetu Mustafa katika uga huu wa kuchapisha hewani pasi na kuwa na mhariri au mchapishaji. Mhariri mkuu na mchapishaji ni wewe mwenyewe.

  Boni kwa mbaali nieanza kupembejeka na neno 'gazeti tando', maana nimeshaanza kuwa na kigagasiko juu ya neno 'blog' kwani mustafa kaita 'globu' sehemu fulani hivi.

   
 • Tarehe 1/28/2006 4:55 AM, Mtoa Maoni: Anonymous nyembo

  Makene!
  sikusalimii hata,nilikuwa nimepanga niseme kitu nawe leo,walakini nimeshikwa na mshutuko wa furaha kwa karibu yako kwa Bwana Mustafa, nimeacha tofauti zetu kwanza ili niweze kumkaribisha mgeni kwanza"karibu Bw. Mustafa!

   
 • Tarehe 1/29/2006 10:57 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Makene poa sana juhudi zako ambazo zimetuletea ndugu Mustapha. Ngoja nimtembelea na kumtangaza.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved