NIMEPITA na kuangukia blogu ya FDC. Hiki ni chama cha siasa Uganda ambapo mgombea wake Urais Kiiza Besigye amekuwa hasimu mkubwa wa Mfalme Yoweri Museveni hadi akatiwa katika hatihati za kusotea segerea. Waweza
isoma hapa na kutoa maoni ya vyama vya siasa na wanasiasa wa Tanzania kufungua blogu zao na kuweka maandishi. CHADEMA ni moja ya vyama Tanzania ambacho viongozi wake wana blogu lakini wote hawajawahi kuweka maandishi humo.
Nimevutiwa na hatua waliyoichukua wanamapinduzi wa Uganda. FDC wanaanzisha njia. Vyama vyetu hasa vya upinzani, vikifuata nyayo hizi, vinaweza kuongeza mtandao wa wanachama nchini.
CHADEMA waimarishe blog yao, wataona matokeo. Maana nguvu ya blog ni kubwa na humo wanaweza kupenyeza sera zao.