Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, January 19, 2006
BLOGU YA FDC

NIMEPITA na kuangukia blogu ya FDC. Hiki ni chama cha siasa Uganda ambapo mgombea wake Urais Kiiza Besigye amekuwa hasimu mkubwa wa Mfalme Yoweri Museveni hadi akatiwa katika hatihati za kusotea segerea. Waweza isoma hapa na kutoa maoni ya vyama vya siasa na wanasiasa wa Tanzania kufungua blogu zao na kuweka maandishi. CHADEMA ni moja ya vyama Tanzania ambacho viongozi wake wana blogu lakini wote hawajawahi kuweka maandishi humo.
 
© boniphace Tarehe 1/19/2006 03:47:00 PM | Permalink |


Comments: 2


 • Tarehe 1/21/2006 8:08 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ibrahim M. Bwire

  Makene, ni njia nzuri ya kuiambia jamii nini cha kufanya, kifanyikacho, na manufaa yake kwa jamii. wanasiasa wa Tanzania na Tanzania yetu ni vema tuykajikita kutafuta maarifa mapya na kuwasambazia wananchi.Uliwahi kuniandikia ukinitaka na kututaka watanzania wote tusome vitabu. nami nimewahi kusema Fikra ni nuru halisi ya akili pevu.Ni kweli wanasiasa wetu wakishindwa kutumia njia hii kuuza sera, kutoa mwelekeo wa demokrasia Tanzania na kuhimiza amani, kufanya kazi kwa kutumia fikra pevu nchi itafika mbali katika anga za demokrasia ya kiuchumi na kisiasa. hima ndugu zetu hii ni njia nyembembe ya kpenyeza nuru ndogo kuangaza giza nene na totoro la elimu ya uraia na wajibu mahsusi wa watanzania. Tatizo ni kwamba kama natumia muda mwingi kuangalia TV, ndivyo unavyoua mawazo mnyumbuliko.

   
 • Tarehe 1/22/2006 1:41 AM, Mtoa Maoni: Blogger Bwaya

  Nimevutiwa na hatua waliyoichukua wanamapinduzi wa Uganda. FDC wanaanzisha njia. Vyama vyetu hasa vya upinzani, vikifuata nyayo hizi, vinaweza kuongeza mtandao wa wanachama nchini.
  CHADEMA waimarishe blog yao, wataona matokeo. Maana nguvu ya blog ni kubwa na humo wanaweza kupenyeza sera zao.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved