Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Friday, December 09, 2005
TUNAKOELEKEA KUBAYA KAMA HIZI NDIZO MAKALA ZA KAMPENI TANZANIA
WANAKASRI, nikusalimu, poleni kwa kunikosa kidogo...ni suala la vimajukumu vinanitinga kwelikweli lakini nimekumbuka kupita kukusalimuni. Katika pita pita yangu nimekutana na makala hii naomba isome mwenyewe kwenye kiunganishi hiki.

Kama hizi ndizo kampeni na lugha za magazeti ya Tanzania nadhani ningeanza kufungia hili kabla sijayatazama mengine. Tazama nyingine hii na isome hadi mwisho. Oooh mbona unaniziba mdomo...samahani sisemi kama ni gazeti la serikali ya CCM. Kama haya ndiyo tunayopanda, siku si nyingi...naomba mnisamehe kutabiri huko tuendako!
 
© boniphace Tarehe 12/09/2005 03:11:00 PM | Permalink |


Comments: 2


 • Tarehe 12/10/2005 6:45 AM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

  Makene,
  Hii ndio taswira kwenye mboni ya jicho letu la habari.Sina mengi kwa sasa,nashiriki kwenye mkutano wa Global Voices,London kupitia IRC.Ila jambo moja tu,sielewi huyu bwana Mhando anachokisema ni nini.Baadaye

   
 • Tarehe 12/10/2005 11:45 AM, Mtoa Maoni: Blogger Boniphace Makene

  Huyo anatukana gazeti unalopigia tarumbeta kule Tanzania na kauli hizi zingeandikwa na Tanzania Daima bila,shaka lingechomwa kabisa na sio kufutwa. Sidhani hata katika Blogu twatoa kauli za bezo na matusi kama hizi kwa wenzetu. Huku ndiko kupalilia kitumbua, mzee mzima kama huyo hivyo sasa kijana mbichi kama mimi nifanye nini? Katu sumu simezani, nipo radhi kitanzini.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved