Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, December 15, 2005
SALAMU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2006 KWA WANABLOGU WA KISWAHILI

Nimetumia neno Blogu hapa si maana nimelihalalisha. Nipo katika vita ya kulikataa. Nafanya hivi kutokana na mbio za haraka kuweka shairi hili na kuzindua mtindo mpya wa kutoa waraka maana nasikia shairi laingia moyoni kuliko utungo wa aina yoyote uliopata kuwepo katika sura za dunia. Haya hili ni shairi lenu wenzangu. Wananchi wa KASRI mwaweza lisoma maana latungwa na Mwanazuo mwenzenu. Haya nisikuchelewesheni...someni uhondo huu!

Nimeamka salama, namshukuru Manani
Amenijalia mema, haki yangu msifuni
Fikira zimerindima, na kunambia kichwani
Wapaswa shukuru hawa, kwa kazi wazofanyani.

Ilikuwa ni ndotoni, kelele nikapigani
Nikataka nipeweni, kompyuta niandikeni
Vina nikavibaini, na kuiweka mizani
Hulka ikanituma, shairi kulitungani.

Asubuhi ikafika, nikafika KASIRINI
Nikahisi nimechoka, uchaguzi kusomani
Mkono ukatamka, wataka kuandikani
Nikaujibu hewala, shairi ninatungani.

Nikenda Jikomboeni, za jana nikaonani
Harakati kafatani, kichwani nikagusani
Nikarudi kwa Mwandani, Kiswahili katajani
Fikra zikanituma, safari mbele kwendani.

Nikaja kwa Bangaiza, naye kaja kimwandani,
Pambazuko kakataza, CHADEMA na uzunguni
Damija naye kacheza, za kina mama wekani
Mkwinda akafanyani, bora weka shairini.

Nikaja kwa Mtafiti, hewala nikaonani
Yeye amejizatiti, Blogu shabikiani
Huyu mama wa matiti, matako kayaanzani
Nikenda kwa tahayari, hofu yangu Mswahili.

Nikashuka kwa Msangi, kakuta kitangazani
Sijui tapaka rangi, kazi yake kuishani
Wa Kutoka Ugogoni, kwa mwezi huja mojani
Sura kaanza kunjani, Mavitu kutoyonani?

Muwakilishi Vyuoni, muoga namsemani
Mengi yapo najuani, kuleta anahofuni
Bakanja yuko mijini, kisifu ivyojengwani
Nikatambua Ngurumo, ni mtu wa msimuni.

Fatma binti Karama, alikuwa kikaoni
Agenda amezichoma, kashindwa kuripotini
Nyembo nikamtazama, picha leo kawekani
Bwaya naye kang'amua, wanasiasa laghai.

Kazonta kabaki wazi, rushwa anaipingani
Marekani mwafatani, Zainaty kahojini
Beatrice kashikani, wanawake ongozani
Nikafika Furahia, bashasha sikupatani.

U wapi ewe Materu, na Mark ulofikani
Njia ninafunguani, salamu zangu wapani
Huyu aliwaagani, kisa likizo kwendani
Sasa anajivunia, mtori kibololoni.

Nitakuwa safarini, kwa Jeff ninaendani
Nasikia kwagandani, barafu poromokani
Mkina sije ombani, wambie rushwa achani
Salamu za mwaka mpya, hapa wazi nawapeni.

Mpo wengi najuani, wachache nimetajani
Msotajwa samahani, haraka yanishikani
Naweza kuandikani, Ottawa nikifikani
Msamaha nipeweni, iwapo nitashindwani!

Naweza shindwa fikani, kuwalisha fikirani
Nendako sifahamuni, kisa radhi kuwahini
Uzima nikutakeni, Mola nguvu wajazini
Nikirudi KICHAKANI, Januari iwe unono.
 
© boniphace Tarehe 12/15/2005 09:35:00 AM | Permalink |


Comments: 8


  • Tarehe 12/16/2005 12:48 AM, Mtoa Maoni: Blogger Egidio Ndabagoye

    Nimekubali kazi nzuri kaka.

     
  • Tarehe 12/16/2005 2:23 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Hakyanani!!

    Da mija.

     
  • Tarehe 12/16/2005 6:16 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Nimekubali. Nimekuhabali. Nimekubali. Nadhani shairi hili itabidi liwe linaendelea kukua kadri blogu za kiswahili zinavyoendelea kukua. Njia nzuri sana ya kuzitangaza zote kwa utamu wa aya bin aya.

     
  • Tarehe 12/16/2005 3:30 PM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Asanteni waungwana kutembelea Kasri lenu. Naona kama muda utaweza kuniruhusu nitajaribu kuwa naweka kitu kama majumuisho ya kila mwezi juu ya fani na maudhui ya Blogu zote kwa Kiswahili. Naambatanisha samahani hii si hoja iliyopitishwa tuombe nguvu ziweze kutimiza hili maana moyo ni dhaifu wakati mwili huu radhi.

     
  • Tarehe 12/16/2005 5:09 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Makene,
    Kuna neno moja nimewahi kulisikia katika kiswahili.Neno hilo ni "gwiji".Sasa kwa walio wengi gwiji ni lazima awe anatembelea mkongojo na bega likiwa limepinda.Kwangu mimi wewe umejitokeza kuwa "gwiji" la wakati huu ambapo sote bado tunaishi.Utunzi mahiri sana huu na achilia mbali kuukubali,nimeupitisha,uende kokote unakoenda.Ahsante!

     
  • Tarehe 12/17/2005 8:05 AM, Mtoa Maoni: Blogger Indya Nkya

    Kaka hapo umeniacha hoi. Kazi murua sana.

     
  • Tarehe 12/17/2005 11:25 PM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    waungwana nawashukuru tena. Nimefika Canada salama na kupokelewa na Mellisa na Emma. Niliyokutana nayo katika safari hii nitayaandika baadaye. Huu ubepari wa Marekani mbaya sana ndugu zangu umenipa wakati mgumu sana.

     
  • Tarehe 1/16/2006 3:56 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    unakazi kubwa sana ya kufikia ushahiri mahiri na wala si ujuaji kutaja majina ya waja hifadhi zako hisia na uchunge ulimio kwani unawaudhi wengi bila ya wewe kujua.

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved