Nipo nami Diamondi, Rais namuonani
Tumekaa kwa makundi, kwa mbele kutazamani
Wamejazana Wahindi, utadhani Uhindini
Moyoni nauguani, kitendawili onani.
Sifa zinatangazwani, kila mtu achekani
Ni mimi nilobakini, machozi ninatoani
Kuna mtu akujani, kwangu nilipoketini
Hasira zamtolani, kisa mimi kuliani.
Namtazama Mkwinda, afike niepushani
Nambiwa nje kaenda, ndani hawezi ketini
Fulana hakuipenda, kwani rushwa yanukani
Wakamwambia huwezi, kuingia ukumbini.
Matangazo yaanzani, Rais kuapishwani
Walombele naonani, suti wamezitiani
Wako wapi masikini,tayari wameachwani?
Kwenye kura tuko sawa, baadaye twatengwani?
Natimka kwa ghadhabu, KASIRINI tuliani
Naona bora kujibu, hoja hii shairini
Hiki wazi kiarabu, ndo kisa sikisomani
Kero sijazisemani, hapa mwanzo naanzani.
Yaliyotokea Zenji, Qudusi atuonani
Mtazirudisha chenji, siku itapofikani
Natangazani rivenji, sina haja kufichani
Sitatumia mtutu, lakini mtajuani.
Nimelisimika jeshi, blogu lafunguani
Hapa hakuna ubishi, naona limeivani
Kwa kasi linashawishi, mawimbi kutimuani
Htutaweza kulala, hadi kazi malizani.
Ndesanjo unafanyani, kikosi kiko mbeleni
Changoja ukipangeni, kazi kianze fanyani
Amri kinatiini, siri yake kushindani
Nani natupa karata, Ndesanjo toa Amri.
Kasirini waingia, wengine watamani
tungu watungia, kuonyesha thamani
kikwete aapia, kwa molawe maanani
nchi kuipa nia, na kuitoa sharini.
Leo ni hii, kesho twaingojea
yajana nanihii, yaleo yatatokea
vijana wapanii, mhanga kujitolea
sifa wampatii, Kiwete wamtolea.
Wazamani wasimteke,wasasa tumomgoze
aonyeshe makeke,vita aiongoze
wahila wasimake, rushwa isitokeze
waume kwa wake,usawa awekeze.
Yamkapa yajulikana,yajakaya hajatia
tusitumie yawajana,mabayani kumtia
akashindwa kulaana,tuwape mkia
ushirikiano nanena,umoja uwepia.
Mkaribisheni dimbani.yetu ayasome
asiwe mkimbizini,kama aliyetokoma
wenzake awabaini,awatoe ulema
wote washibini,wasikate tama.