Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Tuesday, December 20, 2005
NIPO NAMI DIAMOND
Nipo nami Diamondi, Rais namuonani
Tumekaa kwa makundi, kwa mbele kutazamani
Wamejazana Wahindi, utadhani Uhindini
Moyoni nauguani, kitendawili onani.

Sifa zinatangazwani, kila mtu achekani
Ni mimi nilobakini, machozi ninatoani
Kuna mtu akujani, kwangu nilipoketini
Hasira zamtolani, kisa mimi kuliani.

Namtazama Mkwinda, afike niepushani
Nambiwa nje kaenda, ndani hawezi ketini
Fulana hakuipenda, kwani rushwa yanukani
Wakamwambia huwezi, kuingia ukumbini.

Matangazo yaanzani, Rais kuapishwani
Walombele naonani, suti wamezitiani
Wako wapi masikini,tayari wameachwani?
Kwenye kura tuko sawa, baadaye twatengwani?

Natimka kwa ghadhabu, KASIRINI tuliani
Naona bora kujibu, hoja hii shairini
Hiki wazi kiarabu, ndo kisa sikisomani
Kero sijazisemani, hapa mwanzo naanzani.

Yaliyotokea Zenji, Qudusi atuonani
Mtazirudisha chenji, siku itapofikani
Natangazani rivenji, sina haja kufichani
Sitatumia mtutu, lakini mtajuani.

Nimelisimika jeshi, blogu lafunguani
Hapa hakuna ubishi, naona limeivani
Kwa kasi linashawishi, mawimbi kutimuani
Htutaweza kulala, hadi kazi malizani.

Ndesanjo unafanyani, kikosi kiko mbeleni
Changoja ukipangeni, kazi kianze fanyani
Amri kinatiini, siri yake kushindani
Nani natupa karata, Ndesanjo toa Amri.
 
© boniphace Tarehe 12/20/2005 05:25:00 PM | Permalink |


Comments: 3


 • Tarehe 12/21/2005 5:29 AM, Mtoa Maoni: Blogger mloyi

  Kasirini waingia, wengine watamani
  tungu watungia, kuonyesha thamani
  kikwete aapia, kwa molawe maanani
  nchi kuipa nia, na kuitoa sharini.

  Leo ni hii, kesho twaingojea
  yajana nanihii, yaleo yatatokea
  vijana wapanii, mhanga kujitolea
  sifa wampatii, Kiwete wamtolea.

  Wazamani wasimteke,wasasa tumomgoze
  aonyeshe makeke,vita aiongoze
  wahila wasimake, rushwa isitokeze
  waume kwa wake,usawa awekeze.

  Yamkapa yajulikana,yajakaya hajatia
  tusitumie yawajana,mabayani kumtia
  akashindwa kulaana,tuwape mkia
  ushirikiano nanena,umoja uwepia.

  Mkaribisheni dimbani.yetu ayasome
  asiwe mkimbizini,kama aliyetokoma
  wenzake awabaini,awatoe ulema
  wote washibini,wasikate tama.

   
 • Tarehe 12/21/2005 8:34 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Jamani, tuna washairi mimi sikujua. Mloyi, aya hizi bin aya...naona nijitoe nianze kuandika kwa Kichagga sasa. Huwa nasema, "wenye lugha yao waachieni!"

   
 • Tarehe 12/22/2005 4:23 AM, Mtoa Maoni: Blogger mloyi

  Ndesanjo, kwani hesabu hazina washairi? waimbaji?
  hujasikia shairi la kipenyo? Muulize waziri mungai.

   
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved