Tarehe 12/18/2005 5:04 AM, Mtoa Maoni:
Tarehe 12/18/2005 6:49 AM, Mtoa Maoni: Jeff Msangi
Makene,
Karibu sana Canada.Pole kwa usumbufu wa mpakani.Marekani na Canada siku hizi hazielewani vizuri tangu 9/11.Sheria za maingiliano zinazidi kuwa ngumu katika pande zote mbili,hususani kwa wasio wakazi wa kudumu katika nchi hizi.Tuwasiliane unipe programu yako.Ukiweza tafadhali tutembelee huku Toronto
Tarehe 12/18/2005 7:05 AM, Mtoa Maoni:
Tarehe 12/18/2005 10:16 AM, Mtoa Maoni:
Sasa waandikiane kwenye barua pepe ili wafiche uozo uliopo? Bonny hajavunja sheria yoyote na hivyo hapaswi kunyamaza pale anapoona haki yake ya msingi inapokwa. Wewe fikiria masuala ya kukaguliwa mithili ya nini sijui. Kadhalilishwa kinamna. Kama walitaka si wangesema kwa mfano anahitaji viza ya Canada. Bony hakuja Marekani kujipendekeza kama walivyo wengi ambao hawataki hata kujitambulisha kuwa wanatoka Bongo ili waendelee kubanisha Marekani kiharamu. Bony weka humuhumu kwenye blogu (neno sahihi kwa 'blog')
Tarehe 12/18/2005 11:00 AM, Mtoa Maoni: boniphace
Tukinyamaza tutaonyesha tumeridhika na malipo ya madhila. Tukisema twaambiwa tufichiane katika barua za intanenti ili ajue Jeff tu na Mwaipopo. Kwenye Blog tunaandikia nwenzangu ambao hawayajui haya ili wajifunze na wajue kesho yakiwakuta watatue vipi. Huu ni msingi wa hulka njema za Kasri na wakazi wa Zuoni wamepata heshima nyingi kwa Qudusi kutokana na wao kupenda kuwa mawakala wa taarifa njema. Nakumbuka na kukariri tena, nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko
Tarehe 12/18/2005 11:40 AM, Mtoa Maoni: Ndesanjo Macha
Safari njema. Kama kuna theluji huko usiache kwenda kuteleza thelujini. Wewe uliwahi kuteleza kwa kisigino kwenye barabara ya udongo wakati wa masika?
Hizo bugudha za kusachiwasachiwa na kuulizwa maswali ya ajabu ninazifahamu. Ninaelewa kabisa kilichokusukuma hata kuandika. Inaudhi sana. Wao wakija nchi zetu, visa zenyewe wanaomba na kupewa kupitia njia ya posta. Sisi kuingia nchi zao inakuwa kama kosa la jinai. Kinachoudhi kingine ni kile cha kutengwa na watu wengine uwanja wa ndege. Wengine wanaachwa wapite, wewe unaambiwa nenda pembeni. Eti wanasema tarakilishi imeonyesha kuwa unatakiwa kusachiwa kwa undani zaidi...bladifuu!
Haya Mzee Akida tuambie "visa kaisi" ndio nini.