MWANABLOGU wa picha
michuzi amebandika picha inayoonyesha mbio zitakapokamilikia baada ya harakati za kisiasa Tanzania wiki hii inayoanza saa chache zijazo. Ikulu ya Tanzania yeye hapo ameiita White House. Nilipokuwa huko Washington D.C nilipata masimulizi juu ya jina la MAKAO MAKUU YA MAREKANI kuitwa White House. Je
hii ya Tanzania kwa kuwa nayo yaonekana nyeupe yaifaa kuitwa White House au ndio mwendo wa kukopi kila tunachokiona kwa wenzetu?
Hili ningependa nimuachie Michuzi ajibu kwanza.Kutoka kwangu ni pongezi tu za jinsi ambavyo unaweka picha zinazoendana na habari zako.Blogu za namna hii zinavutia zaidi na zinaelimisha kirahisi zaidi.