Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, December 11, 2005
NI IKULU AU WHITE HOUSE?


MWANABLOGU wa picha michuzi amebandika picha inayoonyesha mbio zitakapokamilikia baada ya harakati za kisiasa Tanzania wiki hii inayoanza saa chache zijazo. Ikulu ya Tanzania yeye hapo ameiita White House. Nilipokuwa huko Washington D.C nilipata masimulizi juu ya jina la MAKAO MAKUU YA MAREKANI kuitwa White House. Je hii ya Tanzania kwa kuwa nayo yaonekana nyeupe yaifaa kuitwa White House au ndio mwendo wa kukopi kila tunachokiona kwa wenzetu?
 
© boniphace Tarehe 12/11/2005 03:15:00 PM | Permalink |


Comments: 2


  • Tarehe 12/12/2005 3:40 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Hili ningependa nimuachie Michuzi ajibu kwanza.Kutoka kwangu ni pongezi tu za jinsi ambavyo unaweka picha zinazoendana na habari zako.Blogu za namna hii zinavutia zaidi na zinaelimisha kirahisi zaidi.

     
  • Tarehe 12/13/2005 8:20 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Naona umekosea kiungo cha blogu ya picha ya Michuzi. Kiungo ulichoweka ni cha zamani. Cha sasa ni hiki: http://issamichuzi.blogspot.com

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved