NIMEKUWA katika hamu ya kuona Katiba ya Tanganyika inabadilishwa. Katiba iliyopo haikidhi matakwa ya wengi. Imechoka na kubwa zaidi imejaa viraka. Mfumo wa kuunda sheria Tanzania una ukakasi. Sheria zaanzia serikalini na kisha kupelekwa bungeni kupitishwa. Hakuna kwa dhati kile kiitwacho mgawanyo wa madaraka.
Kuna haya madaraka ya Wakuu wa Mikoa na wale wa Wilaya. Vyeo hivi katika ulimwengu wa sasa havina kazi zaidi ya kuongeza mazingira ua ufalme wa watawala wa Tanzania. Kuna haja ya vyeo hivyo kutumika vingine au kuundwa kwa Bunge lenye sehemu mbili yaani lile la wawakilishi wanaotokana na majimbo yaliyopitishwa kwa uwiano wa namba ya wakazi na lile la pili litakalofanana na kuwa na wawakilishi wa aina ya wakuu wa mikoa au mithili ya maseneta ila hawa wanachaguliwa na wanannchi wa sehemu husika. Hii ni hoja ambayo amekuwa nayo mgombea wa CHADEMA, Freeman Mbowe lakini kwa muundo mwingine.
Kama kutakuwa na wawakilishi wa aina hii kunakuwa na uwezekano wa sheria mbovu zinazogandamiza haki za raia kutopitishwa. Tena ni rahisi kuwa na uwiano wa kimaendeleo badala ya sasa Mawaziri kubadilishia miradi ya maendeleo katika majimbo yao ya uchaguzi ili kujijenga kisiasa na kisha kuyadhibiti majimbo ya wapinzani kwa kuyanyima huduma za maendeleo.
Picha hiyo hapo ni Kongresi ya Marekani ambapo tulitembelea hivi karibuni. Marekani ni moja ya nchi zenye Bunge lenye sehemu mbili. Yaana sehemu ya Wawakilishi na Seneti.
Makene,
Mfumo huu unaouzingumzia hapa ni mzuri sana ingawa lazima tuwe makini sana katika utekelezaji wake.Unajua hawa wenzetu wamedumu kwa miaka mingi sana,wana uhuru wa zaidi ya miaka mia nne sasa.Tanzania bado ni taifa changa sana ukilinganisha na Canada,Marekani au wakoloni wa dunia nzima Uingereza.Lazima tujiulize maswali kama hivi kwanini mfumo tulionao haufanyi kazi?Mfumo wetu wa kiuchumi ni ujamaa au ubepari?