Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Friday, December 16, 2005
JEFF NAJA ! WAWEZA KUNYWA MVINYO NAMI?
SIJAANZA safari bado, itakuwa usiku huu. Siku hizi kuna mengi katika safari hizi na hiki kimekuwa kisa cha mimi kutangaza safari zangu. Utaratibu huu si kwa wabunge na marais tu hata nasi wanazuo tunao ili ijulikane wazi tupo wapi inawezekana kukutana na wale niliowasalimu katika shairi langu hapo chini.

Nitaondoka Edinburg usiku huu na kusafiri kwa Basi hadi San-Antonio. Kesho asubuhi sana nitasafiri kuanzia pale na kupitia miji ya Dallas, Chicago na kisha kushuka Ottawa majira ya jioni. Naamini Insharah Mnyezi Mungu Rabuka atajalia safari yangu kuwa salama. Nikiwa huko nitaweya kuwatembelea ndugu na rafiki zangu. Nitaweza kufika Toronto anakoketi Waziri Mkuu. Naweza kutana naye pale ili sambamba na masuala mengine ni kujadili nafasi ya Blogu za Tanzania katika kuleta mabadiliko ya Kiuchumi na Kisiasa Tanzania siku zijazo.

Kazi hii ngumu sana lakini hatupaswi kuiogopa, sasa ni kama wajibu na tunatakiwa kuifanya kwa moyo mmoja. Jukumu lingine ni hili la kuongeya Blogu za Kiswahili na kuzitangaza. Mlioko ughaibuni mnaweza kusaidia zaidi katika hili na kidogo kidogo walioko nyumbani wataongezeka kwa kasi.
 
© boniphace Tarehe 12/16/2005 03:12:00 PM | Permalink |


Comments: 1


  • Tarehe 12/16/2005 5:02 PM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Karibu sana Makene,
    Namba zangu nadhani hujazitia kapuni.Ukifika Ottawa tuwasiliane.Tafadhali usisahau makoti mazito kwa ajili ya kujikinga na baridi!Karibu Canada!

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved