Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Monday, November 28, 2005
TULIA BABA WAKATI WA KAMPENI BADO

WASHINGTON D.C licha ya kaubaguzi kalikotokana na weusi kunyimwa nafasi ya kupasua anga, lakini kama kawaida utadhani hawakujua nafasi ilimuangukia huyo jamaa mwenye kipaza sauti. Alichofanya ni kutoa yale aliyowahi kuyadokeza katika blogu tukio lililofatiwa na kukubalika kwa furaha sana na Mabalozi wa nchi za Mashariki ya Kati hasa wanaopewa kilema cha ugaidi kutokana na wao kuwa waislamu.

Ilifuata tukio la baadhi ya mabalozi wa nchi hiyo kupata picha ya ukumbusho na mabalozi wa Tanzania huku wakionyesha bashasha kama wanavyoonekana katika picha hii. Huyo hapo chini anayetabasamu ni Ali Lasloom kutoka Saudi Arabia na mwenzake ambaye jina lake halikupatikana mapema anatokea ukanda huo pia.

Jambo lililowasilishwa na Balozi wa Bongo lilikuwa kuhusu kukerwa na tabia za vyombo vya habari vya huku kuwadumaza raia wa huku kiasi kwamba wakadhani Afrika ni sehemu ya vita, njaa na majanga mengine. Balozi huyo alipinga hilo akakakumbushia na suala la Mashariki ya Kati kuhusiana na taabu wapatazo raia wa huko pale wafikapo mataifa ya Ulaya na Amerika.
 
© boniphace Tarehe 11/28/2005 05:38:00 PM | Permalink |


Comments: 1


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved