Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Saturday, November 05, 2005
NITAPOKATA MKIA
NITAPOKATA mkia
Na macho kufunikia
Watu watajatulia
Simanzi uso jazia.

Wachache watatulia
Chini wakitazamia
Wengi watainukia
Moyoni kuchekelea.

Nitataka kusikia
Wimbo huru nipigia
Zeze nitalotolea
Hapana wa kupigia.

Watataka nishikia
Ili uhondo patia
Nami nitakatalia
Thawabu yangu tolea.

Sasa wanatazamia
Kula niliyopandia
Hawataki tafutia
Cha kwao kujijengea.

Wavivu wafikiria
Mali zajaza dunia
Wako radhi kuulia
Wenzao ili patia.

Wamezidi chekelea
Zanzibar Dola shikia
Mtutu wakashikia
Ulaji wao tetea.

Sasa nini mwatakia
Kama si moto washia
Shairi nalotungia
Ndesanjo paswa jibia.
 
© boniphace Tarehe 11/05/2005 03:45:00 PM | Permalink |


Comments: 1


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved