Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Sunday, November 13, 2005
NISEME UKWELI AU NIFUNIKE KOMBE?
KESHO nitaanza kazi za Ubalozi wa Tanzania hapa Marekani. Nitakuwa na wiki ya mihangaiko ya kuitangaza nchi hii. Awali jitihada zangu za kutaka kuweka nguvu zaidi katika kuitangaza Tanzania zilikwamishwa na hawa tunaowalipa na wanakaa pale Washington DC wakijiita Ubalozi wa Tanzania Marekani. Sisemi hasa hapo maana niliandika wiki iliyopita.

Nitakuwa na kibarua cha kuzungumzia Tanganyika maana hiyo Tanzania kwanza bado hawajatoa maandishi ya mkataba wake. Sheria za Tanzania haziruhusu kujadili suala lililopo mahakamani kwa hiyo nitaizungumzia zaidi Tanganyika. Kisha nimekumbuka, hakutakuwa na mtu wa kuitangaza Afrika, nitajitwisha jukumu hili pia!

Nadhani sina kosa kukumbusha kuwa sina Bendera ya hiyo Tanzania. Tena afadhali maana ni juzi juzi tu huko huko Bongo wakazi wa Bukoba wametoa kali pale walipoamua kuandamana na bendera ya Marekani. Patamu sana hapo, nadhani hawakuwa na Bendera ya Tanzania maana kibali cha kuipata anapaswa kutoa Mapuri na inatolewa kwa masuala maalum.

Chama cha CUF kwa sasa naona hawawezi kabisa kuipata hiyo, cha kufanya wameamua kuonyesha utata unaotukabili Watizedi tyulio nje juu ya kukosekana bendera zetu. Nitazungumkwa na wawakilishi wa mataifa mengine, najua nitawafunika kwa maelezo lakini hili la Bendera nitahaibisha. Nitajifanya sijui kusema nimeona nisichukue bendera yangu kwa kuwa nawakilisha bara la Afrika lakini nao wataniomba walau ile ya AU.

Sikuwahi kuioana hata hiyo, nilisahau walau ningemuomba Mtikila aniazime ile ya Tanganyika siku nilipokuwa kwake nikamkuta anaweka mpya na kushusha ile nzee. Sijui kwa nini nilisahau! Kazi ipo!

Baada ya mambo ya kazi za wiki hii nitaaanza safari za kwenda Washington DC, nitaandika nitakayoyakuta huko hapa. Kisha nitarejea New York hapo napo nitasema jicho langu limeona nini. Sitaishia hapo nitafika hadi New Jersey kabla ya kurudi Washington na kuanza safari ya kwenda Texas Houston. Huko kuna kingine, nitakutana na wadanganyika wenzangu siku ya "THANKS GIVING". Tutakunywa mvinyo na kisha nitapata fursa ya kuwasikia na kutoa sera zangu. Nikimaliza kesho yake itakuwa safari ya kuja hapa Edinburg. Nifikapo kuna kazi ya kuanza kutoa darasa la Utamaduni wa Mwafrika na lugha yake Kiswahili. Ee Mungu nisaidie.
 
© boniphace Tarehe 11/13/2005 01:25:00 PM | Permalink |


Comments: 5


  • Tarehe 11/14/2005 2:00 AM, Mtoa Maoni: Blogger Indya Nkya

    Pole kwa kufanya kazi ngumu namna hiyo. Kutangaza nchi ngumu kama ya kwetu. Kazi tunayo. Hizi ofisi za ubalozi za Tanzania nchi zote zina tatizo. Sijasikia mtanzania anayejivunia ubalozi wake. Nadhani suala linaeleweka. Wapo kuvutia wawekezaji weupe. Wakiona ngozi nyeusi inayoongea kiswahili ni nuksi nuksani. Kazi tunayo

     
  • Tarehe 11/14/2005 6:05 AM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Ukifika pale DC kawazabe vibao vya harakaharaka jamaa pale ubalozini!

     
  • Tarehe 11/14/2005 6:35 AM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Idya nashukuru na pia pole kwa usumbufu huo nilioufanya bila kutarajia. Niliwahi kusoma maoni ya mtu huko nyuma akiwa kaandika kama hivyo nami bila kujua nikajikuta naingia katika mkenge huo. Hiyo makala ya mwenye nyumba ina ukweli ndani yake, na kuna jambo limeanza kutokea huko Tanzania.

    Pia Ndesanjo nitajitahidi kufika pale na sitaki kuwapa taarifa za awali maana lazima niwaone kisha niwaandike upya sasa.

     
  • Tarehe 11/14/2005 8:56 AM, Mtoa Maoni: Blogger Indya Nkya

    Usijali Makene. Tuendelee kupambana na hawa jamaa wasiojua cha kufanya. Wanadhani ubalozini ni kwenda kutalii na kuongea na ngozi nyeupe. Tutawachapa makofi kwa kalamu.

     
  • Tarehe 11/14/2005 5:43 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    Hapana Makene tunaweza tu tukawa na vazi la Tanzania, kunradhi nilitaka kutamka Tanganyika ila ulimi umeteleza kidogo tu. Au tunaweza tukawa na mavazi ya taifa ya aina mbili ama tatu kutokana na tabaka halisi la mwananchi husika. Wazo langu tuanzishe vazi la magunia kwa tabaka la akina pangu pakavu tia mchuzi. Nafikiri hatutatakiwa kuwa na passport kupata magunia kama yale ya iliyokuwa nesho milingi. Au unasemaje.

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved