Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Friday, November 04, 2005
MCHEZO WA MASKINI JEURI WA ZANZIBAR MWENYE UCHU WA MADARAKA YENYE UTATA
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeperwa tamko la jumuiya ya NDI sambamba na Ubalozi wa Marekani Tanzania kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar uligubikwa na utata ukiwemo ule wa wizi wa kura na usiri wa zoezi hilo.

SMZ kama kawaida imekuja na kasi ya kupinga ikiegesha ushaidi wake kwa taasisi zilizokuwa chini yake moja ni ile inayoongozwa na Profesa wa CCM, Mkandala yenye makao makuu yake Chuo Kikuu Mlimani, TEMCO, nyingine ni ile inayoongozwa na akina Mkapa yaani ya SADC, na ile ya AU.

Ukiziangalia hizi zote zimeshindwa kumsaidia hata Mugabe aliyefanya jambo la kishujaa baada ya kuona upatikanaji wa kura unapotea. Hawajamsaidia kifedha na raia pale wanakufa kwa kukosa chakula. Sasa hao hao walioleweshwa mvinyo hapo Bongo wameibuka na sasa wanatumika kama reference ya SMZ dhidi ya taifa kama Marekani.

Naona hawajui hawa jamaa kuwa Marekani sasa inaongozwa na Republican. Hawajui hawa jamaa namna Marekani ilivyobadilika sasa kama mkondo wa taarifa zake ukifika katika Congress. Bush aweza tenda lolote kwa sasa na baya ni kufutiwa misaada na kama Marekani ikitangulia sijui atafuata nani?

Naona busara zinatakiwana huu ndio wakati wa Mwalimu Nyerere Foundation kuchukua mkondo kuweka sawa pande hizi. Yu wapi Salim Ahmed Salim na mwenzake Warioba, anzeni kazi sasa msingoje mambo yawe hatari. Fahamuni uchu wenu wa fisi ni mauti ya umma unaowazunguka, mtahukumiwa kwa kuficha ukweli uliowazi.
 
© boniphace Tarehe 11/04/2005 10:45:00 AM | Permalink |


Comments: 1


  • Tarehe 11/05/2005 7:34 AM, Mtoa Maoni: Blogger Indya Nkya

    Profesa wa CCM!! Umegonga msumari kwenyewe. Anapotaka kuitetea CCM anasahau kabisa kwamba yeye ni mtaalam. Wakati mwingine hukiuka hata taratibu za tafiti ili kutetea Chama chake.

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved