Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Wednesday, November 23, 2005
Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2005
Kuna msomaji amenitumia maandishi haya, nimeona niyabandike bila kuyachafua wala kupunguza chochote. Mwaweza kusoma na kuwasiliana naye kwa maandishi zaidi.
.............................................................................

Ni Tamaa ya Jamii ya Tanzania mbele na Mauti ya Wahisani na CCM Nyuma

Wakati wa kugombea uhuru wa Tanzania, wapiga kura walibeba vyama vya siasa na TANU mgongoni na kupigana ana kwa na ubeberu wa mabepari duniani kwa sura ya utawala wa Waingereza. Mabepari wanaoandamwa na madhambi ya utumwa wa miaka 350 na ukoloni wa miaka 150 duniani. Kwenye uchaguzi wa 2005, wapiga kura wa kizazi kipya watakuwa wamebeba vyama vingi vya siasa mgononi na kupigana tena ana kwa ana mabepari wa dunia kwa sura ya wahisani wakiwa wamebeba rekodi ya TANU/CCM mgongoni kwa miaka 40
Kuanzia mwaka 1965, wapiga kura wa Tanzania wamekuwa wakikokotwa kwenye maigizo ya uchaguzi mkuu kila baada ya miaka mitano kwa mara tisa na kwa miaka 40. Matoke ya maigizo haya ya kuweka mbele tamaa na madhambi kuhalisha ushindi wa wahisani na TANUCCM na kutosa kuwa nyuma mauti ya jamii. Matokeo ya uchaguzi mkuu 2000 yatakuwa ya ushindi wa tamaa ya wapiga na jamii kuwa mbele na mauti ya wahisani na CCM kuwa nyuma.
Tamaa na lengo kuu la wapiga kura wa Tanzania ni kuhakikisha kwamba wana maisha bora kwenye ushindani wa maendeleo duniani kwa kuchagia viongozi safi wa utendaji bora wa utawala wa jamii. Tamaa ya viongozi wa TANU/CCM na wahisani ni kuhakikishia kwamba wanaendesha utawala wa nchi milele kwa njia yeyote ikiwa ni pamoja na mauti ya jamii. Lengo lao kuu ni kumiliki uporaji wa mabepari wa mali na nguvu kazi ya jamii na taifa. Ili kufanikisha tamaa yao, viongozi wa CCM wamekuwa wakukokota wapiga kura na vyama vya siasa kwenye maigizo ya uchaguzi mkuu ili kuhalalisha utawala wa madhambi na mkataba wa kuwa tegemezi wa kupindukia kwa wahisani wa nje na ndani ya nchi.
Wakati wa uhuru, miaka 44 iliyopita chama siasa pekee cha TAMU/CCM kiliweka ahadi na kiapo mbele ya jamii cha kuwajibika na utendaji safi na bora wa utawala wa jamii kwa kujikomboa na kuleta maisha bora. Viwango na vigezo sahihi vya kimataifa na hali halisi ya maisha vimedhibitisha kwamba jamii ya Tanzania hajapata maendeleo hapa duniani kwa miaka 30 iliyopita, wamebaki kundi kwenye kundi la chini na mamba 164 au wa 14 kutoka mwisho. Leo hii, waliokuwa adui wa maendeleo wakati uhuru; ambao ni umaskini magonjwa na ujinga wamekuwa mauti na majanga ndani ya jamii ya Tanzania. Kiwango cha maambukizi ya Ukimwi ni asilimia 7 ambacho ni cha juu sana. Takriban watu 1.5 milioni ni wamekufa na Ukimwi na wengine 1.5 milioni wanaisha na virusi.
Mwaka 1965, viongozi wa TANU walivunja kiapo kwa kufanya dhambi ya kubadili utendaji wa utawala wa jamii kutoka mfumo wa vyama vingi vya siasa na kuanza wa chama kimoja bila ridhaa ya wapiga kura na jamii. Ikawa jamii haina sauti na kauli yao chombo na kutoswa kwenye mauti. TANU ikakumbatia wahisani na madhambi ya kuwa tegemezi. Jamii ikatoswa tena mwaka 1967. TANU ilibuni na kutekeleza Azimia la Arusha na itikadi na sera mpya ya ujamaa na kujitegemea bila ridhaa yao. Kinyume kabisa na kwa siri kubwa, viongozi wa TANU/CCM waliongeze kiwango cha kuwa tegemezi kwa wahisani mara saba. Mwaka 1986, viongozi wa CCM wakavunja Azimio la Arusha kisisiri na kuweka mkataba wa kuwa tegemezi wa kupindukia na kuhamia mgongoni kwa wahisani na tena bila ridhaa ya jamii
Leo hii, viongozi wa CCM hawana itikadi na sera sahihi ya kusimamia utawala na kuhakikisha ukombozi, maisha bora na maendeleo ya jamii duniani. Taifa huru la Tanzania lina janga kuu la utawala wa maovu na mbovu chini ya viongozi wa CCM wa kuhakikisha mauti ya jamii. Hawataki kuwajibika na madhambi ya kuvunja kiapo mara tatu na kuleta mauti kwa muda mrefu wala kuiga mfano wa kuwajibika kwa waasisi wao Wenyeviti na Rais Nyerere na Rais Mwinyi.
Lengo kuu la viongozi wa CCM na wahisani ni kuhujumu, kumiliki na kudhibiti kikamilifu mihimili ya Vyama vya Siasa, Wapiga Kura na Tume ya Uchaguzi ambayo ni nyenzo za ujenzi na utendaji wa utawala sifi na bora wa jamii.
Tamaa ya viongozi wa CCM ni kuhakikisha ni kuwa chama namba moja kwenye Sheria mbaya ya vyama vingi vya siasa. Pili ni kutosa Vyama vya siasa wa kuvipa ruzuku za uchwara kwa hadaa ili mradi washiriki maigizo ya Uchaguzi Mkuu. Tatu ni kuweka mawakala wao kwenye Tume ya Uchaguzi ili kujihakikishia ushindi wa kishindo. Nne ni kutoa takrima na kukokotwa kwa wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu bila wao kuelewa itikadi na sera za vyama au ubora, usafi, madhambi na ubovu wa wagombea. Tano ni kudhibiti waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi na kukejeli ukweli wa taarifa zao. Woga mkubwa na mauti ya wahisani na CCM kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa haki, huru na usawa.
Hakuna tena uwezekamo wa chama cha CCM kuwajibika na madhambi ya kuhakikisha halaiki ya mauti kwa jamii na kuachia kugombea uongozi ili kuepusha mauti kwa jamii kwa miaka mingine mitano na jumla ya miaka 45. Miaka 45 ni karibu maisha yote ya Mtanzania duniani. Mpanda ngazi kushuka au kuanguka. Dunia tusiifanye maisha ya tupa. Ni wazi kwamba viongozi wa CCM wameshindwa kukomboa jamii na majanga na kuleta maendeleo yao duniani.
Ukurasa mpya wa kuhakikisha tamaa na ukombozi wa jamii Tanzania umefunguliwa. Vyama vingi vya siasi na waandishi na vyombo vya habari, viongozi wa duni na vyama vya jamii na wataalamu ambao siyo mawakala wa madhambi ya viongozi wa CCM wana wajibu na jukumu la kuhakikisha ushindi wa wapiga kura na jamii wa Tanzania. Vinginevyo historia itawaadhibu.
Wawapiga kura wa wajibu mmoja ambao ni kuchagua viongozi SAFI wa kujenga utawala BORA na mpya utakaolinda kiapo cha kuhakikisha kujikomba na kuleta maisha bora kwa jamii. ya Tanzania. Wapiga kura peke ndio wenye uamuzi na kura yao, ambayo ndiyo silaha ya kuwakomboa. Wapiga kura wa Tanzania watakuwa wamefanya makosa mara 8a kila baada ya miaka 5 na wamepewa adhabu ya kulipa kwa mauti na majanga kwa jamii yao kwa miaka 40. Kufanya kosa siyo kosa, lakini kurudia ni kutoa hukumu ya maisha duni na taabu, mauti, majanga kwa watu 41 milioni wa Tanzania.
Haya shime wapiga kura wa Tanzania, maigizo ya uchaguzi mkuu yamefika mwisho. Kuchagua ni kupanga na kupanga ni kuchagua. Anzeni milenia mpya ni ya kujihakikisha tamaa ya kujikomboa na maendeleo duniani kwa jamii ya Tanzania daima iko mbele na ili ya madhambi ya wahisani na CCM na mauti iko nyuma yenu.

Dk.. Godfrey B .R. Swai.
Mtafiti na Mshauri Mzalendo wa Afya na Ustawi wa Jamii
E-mail jikomboe2000Afrikusa @yahoo.com
 
© boniphace Tarehe 11/23/2005 05:31:00 PM | Permalink |


Comments: 0


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved