Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Monday, November 14, 2005
MAKOFI NA NDELEMO, MAONYESHO YA MAVAZI
NIMETOKA sasa kuonyesha vazi langu.Hili ni tamasha la wiki ya kimataifa hapa Chuo Kikuu cha Texas Pan American. Makofi yalikuwa mengi na shangwe utadhani nagombea cheo fulani cha kisiasa. Nadhani makofi haya yanashiria namna ninavyokubalika...ooh samahani namna nilivyokuna vichwa vya hawa wadhungu kwa haka kavazi kangu!

Nilipotoka tu nikadakwa na Mwandishi wa Habari wa gazeti maarufu hapa, Laitwa The Monitor aliwahi kufanya mahojiano nami huko nyuma na kuyachapisha katika gazeti hili hapa.

Ananiuliza nimejisikiaje kuwakilisha, Swali tamu sana kwangu, namjibu, fursa hii kila binadamu huomba Mola ajalie kuipata. Niliwahi kuwaza lini nitawakilisha nchi yangu lakini Mola kanijalia leo kuwakilisha Bara zima la Afrika. Kama ni majukumu nzito na kubwa nipate nini zaidi ya haya. Limebaki moja tu sasa nadhani, kuwakilisha Ulimwengu na sijui itakuwa wapi, yaweza kuwa Mbinguni...oooh si huko nitakuwa nimekufa tayari?

Nadhani njia ni hii moja ya kuwawakilisha walimwengu na kugeuza dunia uwanja usio na mipaka. Ulimwengu unatakiwa kuwa Kasri huru lenye kuruhusu kila mmoja kuingia na wala si hili la Mwanazuo ambalo lataka wenye kupenda kula fikra!

Kesho Jumanne nitakuwa na kazi ya kuchonga, nitakuwa pamoja na ndugu yangu toka Saudi Arabia. Msiwe nna shaka waungwana inapofika uwanja huo, tayari nilishafunika! Nitafika hapa baada ya wakati huo ila tu naona mashabiki wanazidi kuongezeka na wanaweza sasa kunitamka kwa jina. Ee Mungu nifanye nini mja wako. Nabaki kumshukuru na kumuomba awabariki kila mlitembeleapo Kasri hili.
 
© boniphace Tarehe 11/14/2005 06:24:00 PM | Permalink |


Comments: 1


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved