Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Wednesday, November 16, 2005
MABOMU NI DEMOKRASIA YA AFRIKA?
MWANDISHI mmoja wa gazeti la Mwananchi amenitumia habari kuhusu wasiwasi unaoikumba Uganda sasa. Kila kona ni mabomu mathalani baada ya mgombea wa Upinzania kukamatwa na Polisi siku chache zilizopita na kutiwa korokoroni. Kiiza Besigye alitangazwa mapema kuwania Urais na wiki chache tu baada ya heshima hiyo akatiwa pingu.

Mashabiki wake hawataki kuamini kuwa inawezekana suala hili halina uhusiano na hujuma za Museveni yule Mfalme wa Uganda. Sambamba na hilo kuna mgomo mwingine pale Chuo Kikuu Makerere, chuo kilichofurika umati wa wanafunzi waliosongamana mithili ya njugu, hawa wanadai kupanda kwa gharama huku maisha yao yakiwa chini. Katika chuo hicho kuna kundi la vijana wanaokula maisha ya haki ya serikali na wengi kubaki na udhamini binafsi.

Wakati haya yakiendelea, nipo katika harakati za kuiwakilisha Afrika na siku zijazo sitakubali kufunika kombe nitapasua ukweli kuwa Mabomu na vitisho ndiyo demokrasiua ya wafalme wa Afrika.
 
© boniphace Tarehe 11/16/2005 06:26:00 AM | Permalink |


Comments: 0


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved