
NI juzi nimepata waraka kutoka katika kaboksi kangu ka barua za intaneti kutoka ubalozi wa Marekani. Waraka huo unazungumzia na kunikumbusha kuwa safari yangu sasa inafikia mwisho na hivyo napaswa kujiandaa kufungasha vyangu na kukaribisha wengine watakaokuja kuchukua mikoba yangu mwakani. Sina cha kufungasha hapa, sikupata uwezo wa kununua mashamba kama Fredrick Sumaye, similiki magari na wala sina fedha ina nina utajiri mkubwa wa fikra kuliko nilivyokuwa hapo awali.
Siku hizi naweza kusema bila kuogopa, naweza kulitamka jambo baada ya kulitafiti, nafahamu madhambi ya mataifa haya makubwa na kubwa ninawajua watu wake kama wanifahamuvyo. Nawakaribisha wote wanaotaka kuomba ajira hii kama wana sifa soma hapa kwa maelezo zaidi.
Makene, asante kwa kutupatia picha kebekebe. Kiungo hapo juu naona kina makosa fulani.