Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, October 06, 2005
WANATAKIWA AKINA MKONO WENGI AWAMU YA NNE!

Kwa mara ya kwanza nimeanza kuona sura za Mwalimu Nyerere wengine Tanzania. Viongozi wasioogopa mazingira ya ugumu na badala yake wanakubali kukabiliana na matatizo yanayowakabili wananchi.

Nilmud Mkono ni mbunge wangu kwa vipindi viwili kimoja kimekwisha na kingine natambua watamuongezea. Baada ya hapo atanipisha, lakini kwa mkondo huu anastahili pongezi. Nitaandika juu yake baadaye lakini sasa fahamu hilo tu.
 
© boniphace Tarehe 10/06/2005 04:07:00 PM | Permalink |
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved