Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, October 20, 2005
UTUBORA, UJINGAHASARA
NIMESOMA jana kitabu cha "Kufikirika" cha Shaaban Robert. Sikuwahi kukisoma hiki licha ya kuwa nilitarihi kile cha Kusadikika. Kitabu hiki ni moja ya nguzo za busara mbazo nadhani Mkuu wa Mkoa wa Tanga anatakiwa kusoma. Huyu namshauri asome pia hiki cha "Sanaa ya Ushairi" ili asome shairi la Tanga na hapo atapata jibu la juu ya hoja yake ya kufungia wimbo wa Rapu wa Tanga Kunani ulioimbwa miaka kadhaa nyuma na Wagosi wa Kaya.

Mwingine ninayemtaka kurejea vitabu hivi ni Mfalme Mungai na Babaye Mkapa. Wasome hivi vitabu, "Kufikirika na kisha Kusadikika wakimaliza kabla sijawapa test wasome Nagona na Mzingile vya Profesa Kezilahabi. Hivi viwili vya mwisho vyaweza kuwa vigumu kwao, wanaweza kuniomba niwape fasili rahisi ili wavielewe vema.
 
© boniphace Tarehe 10/20/2005 01:32:00 PM | Permalink |


Comments: 3


  • Tarehe 10/26/2005 9:07 PM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Hujakosea. Nagona na Mzingile wakivianza watavimaliza baada ya miaka 21, tena kwa kiboko. Na kingine ni Karibu Ndani cha huyo huyo Kezilahabi wa zile enzi za Rosa Mistika, Gamba la Nyoka, Dunia Uwanja wa Fujo. Rosa Mistika tulikuwa tukikisoma chini ya shuka!

     
  • Tarehe 10/27/2005 9:44 AM, Mtoa Maoni: Blogger boniphace

    Natambua hivyo Ndesanjo, hawa jamaa wanafanya mambo ya aibu sana na huwewzi kuamini kuwa kazi za Shaaban Robert sasa ndio zinaonyehs akufanya kazi katika Tanzania. Uandishi wa Kezilahabi unahitaji uwepo na nuru ya kuona, nafahamu Mkapa haoni tena, kawa kipofu nasukumwa na kukubali kila wanachosema hao anaodhani wana uwezo finyu kama wake

     
  • Tarehe 10/31/2005 8:55 AM, Mtoa Maoni: Blogger Indya Nkya

    Mkapa ni wa kusaidiwa jamani. Saa nyingine naona tunategemea makubwa kwa mtu ambaye ndio mwisho wa upeo wake. Kumuomba chura mkia. Atautoa wapi?

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved