Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Tuesday, October 11, 2005
TANZANIA YA SASA

Niliamka jana mapema baada ya kusoma sana usiku. Leo nimefika hapa na kukumbuka kuwa sijaweka maandishi kabisa. Kwanza nasikia kauli za kufungia kila kitu zinazidi kukua hapo Tanzania. Nadhani umefika wakati wafalme wa Tanzania wawatangazie akina mama kuwafungia kuzaa watoto vichaa kama Boniphace Mazega Makene.

Hili wanatakiwa kulifanya sasa maana nyimbo tunazoimba sasa hatutakubali kuona zinafungiwa. Sitakubali katu kuangalia wafalme wanageuza nchi mali yao huku wanajifanya sasa kuomba kura. Kusifia matukio ya ufalme kunanipa kichaa kabisa na kumuona Mfalme Mkapa kuwa hana chake ngoja siku za vijimadaraka vyake vikamilike. Natambua wamechuma, na vijana wake wanakenua vijino sasa.

Mwisho si mbali vitarejea tu kwa Watanzania wenyewe kwani huwawezi kuishi karne nyingi. Naweza mimi kuishi kwa kutunza fikra hizi miaka hata miaka lakini mali yatapotea tu.
 
© boniphace Tarehe 10/11/2005 10:09:00 AM | Permalink |
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved