Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Saturday, October 15, 2005
NIPO HOUSTON, TEXAS
NIMEFIKA hapa leo na kukutana na ndugu zangu kutoka TANZANIA. Safari ya kuja huku ina lengo la kujadili masuala ya kisiasa na namna ya kujipanga kusaidia umma wa watanzania. Mazungumzo haya ya leo yanaongozwa na mtaalamu wa Udaktari anayesomea masuala hayo hapa Marekani, Mwandishi na mwongoza Picha za video na Televisheni anayechukua shahada hiyo hapa Marekani, mtaalamu wa masuala ya Kisiasa anayesoma na kufundisha hapa Marekani, na mtaalamu mwingine wa masuala ya Upasuaji naye hapa Marekani.

Mazungumzo haya yatawafurahisha sana hawa: Baraka Mraha, Selestine Kakele, Nehemia Mandia, Gasper Materu na wengine siwataji kwa sababu muhimu. Fuatilia makala zangu katika Mwananchi kupata visa hivi na wale mnaonipata hapa subirini wiki kesho maelezo zaidi.
 
© boniphace Tarehe 10/15/2005 11:01:00 PM | Permalink |


Comments: 3


  • Tarehe 10/15/2005 11:46 PM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Boniphace,
    Karibu mwana kwetu. Nimo ndani ya Kasri lako dakika hii. Hongera kwa kuingia kwenye ulimwengu wa blogu.

     
  • Tarehe 10/16/2005 2:18 AM, Mtoa Maoni: Blogger Indya Nkya

    Karibu Makene. Twasubiri mengi.

     
  • Tarehe 10/16/2005 9:04 AM, Mtoa Maoni: Blogger Jeff Msangi

    Makene,
    Karibu sana kwenye uwanja huu wa mapambano yasiyo mtutu wa bunduki ingawa ni makubwa kuliko vita zote.Si unajua ule msemo wa kizungu usemao A pen is mightier than a sword?Karibu sana

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved