Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, October 20, 2005
NGUMI, NDITA, MAKUFURI BODI YA MIKOPO
Dar sasa vituko mtindo mmoja. Inahitaji kwenda jim au kubeba vitu vizito. Huwezi kuamini umati wa wanafunzi walivamia hivi karibuni makao makuu ya Bodi ya Mikopo na kisha kufunga makufuri ili hadi mikopo yao itakapowekwa kwenye akaunti zao.

Bodi hii imenipa faraja maana inawaunganisha sasa wanafunzi wa Tanzania na siku sio nyingi watapigania haki zao kwa nguvu. Naliona hilo maana licha ya fedha kichele wanayopata sasa lakini inacheleweshwa na kuwekewa mizengwe. Najua siku si nyingi wataungana kugoma na kuandamana kudai fedha nyingi zaidi.

Haya wakati wanafunzi wanawaza hivi wafanyakazi katika Tanzania hasa Walimu, Polisi na Madaktari mnasubiri nini! Hamuoni hayo mashangingi ya wabunge na wafalme wa mawizara. Mnadhani wanamwaga rushwa sasa kwa sababu ya kumpenda nani? Amkeni sasa angalieni namna njema ya kujipanga na kujijenga huku mkiijenga Tanzania.

Ugumu wa maisha haukupangwa kuwa mhimili wa maisha ya Watanzania. Wengi tumechoka kuona watu kadhaa tu ndio wanaoneemeka kama walizaliwa wakiwa wafalme. Nachoka kuandika, hili na sina nia ya kuchochea lakini sijali huu ni wajibu wangu. Hakuna haja ya sisi kubana mikanda wakati akina Mkapa na wenzake wanalegeza ya kwao kufuatia kunona na kodi zetu na raslimali wanazogawa bureeeee tena mchana mchana.
 
© boniphace Tarehe 10/20/2005 01:07:00 PM | Permalink |


Comments: 0


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved