Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Monday, October 31, 2005
MAMBO YAANZA, DAR YAZIZIMA, POLISI, MITUTU MABOMU ZENJ
JANA kuna makundi kadhaa ya watu waliopelekwa kwenye maroli kupiga kura Zanzibar. Walitokea wapi? Wakazi wa vituo halali walikana kuwafahamu na waandishi wa Habari walipowauliza hawakufunua vinywa vyao kutoa majibu! Kazi yao ikawa kuingia ndani ya vituo wakilindwa na FFU ambao waliwatawanya raia halali wa vituo hivyo kwa mabomu ya machozi!

Baada ya matukio kama hayo kukafatia, njama ya kihuni ya kuteka walinzi wa mgombea wa CUF, Maalim Seif na kisha kutoweka huku Polisi wakikana kupata taarifa hiyo wakati Seif alipiga simu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kumueleza pamoja na IGP, Mahita.

Jijini Dar es Salaam maelfu ya mashabiki wa CUF, wakaamua kuandamana na hii inatoa picha namna athari ya mchezo wowote utakaofanywa unavyoweza kuiathiri Tanzania na kuigeuza ardhi ya mauaji yasiyo na umuhimu kama jitihada za kuhepusha hali hiyo zipo. Maandamano hayo yaliendana na vurugu kadhaa huku pia Polisi wakitumia nguvu kuyatuliza.

Matokeo ya awali yaliyoanza kutoka yakaonyesha kuwa CUF wanazidi kuibwaga CCM kwa mbali mno. Lakini mapya ni haya.....tena sikio sasa na pita kwenye blogu hii mara kwa mara!
 
© boniphace Tarehe 10/31/2005 06:56:00 AM | Permalink |


Comments: 2


  • Tarehe 10/31/2005 2:06 PM, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

    Endelea kutupa yanayojiri. Watapona walalanjaa mwaka huu na hayo mabomu na marisasi?

     
  • Tarehe 10/31/2005 7:15 PM, Mtoa Maoni: Blogger Boniphace Makene

    Ndesanjo niarudi hapa asubuhi, kutoa yaliyojiri lakini hakuna furaha kabisa kama nchi yetu inakwenda hivi, Ee Mungu tusaidie tuepuke damu hii inayokuja kumwagika sasa

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved