Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Friday, October 21, 2005
MAKALA YA SAM NA MZOZO BODI YA MIKOPO
Mikopo yazua balaa!
Sam Kamalamo

Jumanne ya Oktoba 18 mwaka huu, nilijikuta niko kwenye Ofisi za Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu (HELB) zilizoko Msasani katika eneo maarufu lijulikanalo kama TIRDO. Kilichonipeleka TIRDO siku hiyo asubuhi majira ya saa nne si kitu kingine, bali kufuatilia mkopo nilioomba ikizingatiwa nilifikisha fomu zangu katika ofisi hizo tangu Agosti 10 pasipo kupata majibu huku waliopeleka nyuma yangu wakiwa wamepata hiyo inayoitwa mikopo.

Kama ilivyo ada, eneo lile tangu kuanza kwa vurugu zakufuatilia mikopo limekuwa halikauki wanafunzi. Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchi hukusanyika kila kukicha kutaka kufahamu hatima ya mikopo waliyoomba.

Wako baadhi ambao wamelazimika kuacha masomo yakiendelea vyuoni kwao na wao kuputeza muda TIRDO. Nikisema kupoteza muda nakosea, wanatafuta haki yakuandikishwa vyuoni kwa vile bila mkopo hakuna mtoto wa masikini anyekanyaga darasa.

Nikiwa katika ofisi hizo kwenye majira ya saa tano nanusu asubuhi, ghafla likaingia kundi la wanafunzi kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (Tanzania Instituteof Accountancy- TIA), wakiwakiimba nyimbo mbalimbali na huku wakiwa na mabango. Baadhi ya mabango yalisomeka “Hakieleweki kitu hadi tupate Mkopo”, “Tunataka kukutana na Mwenyekiti” na maneno kadhaa wa kadha.

Wanafunzi hao wake kwa waume, walijongea hadi kwenye lango la kuingilia ofisini, TIRDO, hivyo ofisa wa bodi aliyekuwapo mlango akalazimika kuusindika mlango huo wa chuma “grill”. Hiyo haikuwa dawa.

Wanafunzi hao wa TIA waliendelea kuimba na kushikiza kuonana na Mwenyekiti wa Bodi Nimrod Mkono ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Vijijini tiketi ya CCm anayewania kurejea madarakani katika uchaguzi wa Oktoba 30 mwaka huu.strong>Mkono hakuwapo TIRDO, lakini wanafunzi wa TIA walitaka kushinikiza kuhakikisha anafika mahali hapo kama alivyofika pale wanafunzi wa UDSM na IFM walipokusanyika kwa nyakati tofauti.

Walipoona hoja yao haisikilizwi, waliamua kuzigeuza ofisi hizo jela kwa muda, pale mmoja wao alipokuja mbele na kufuli aina ya Solex na kufunga hizo grill kwa nje. Kweli ilikuwa jela. Wengine tulijikuta tuko jela kwa mara ya kwanza pasipo kufanya kosa lolote la jinai. Kutoka kwangu jela mapema kulichangiwa na waandishi waITV waliofika eneo hilo kwa ajili ya kuchukua stori.

Usiulize walinisaidiaje. Kimsingi maandamano yale ya wanafunzi wa TIA yalitokana a ukweli kwamba baadhi yao majina yameonekana kwenye hizo wanazoita batch, lakini pamoja na kuonekana kwa majina fedha hazikuwa zimeingia kwenye akaunti zao, hivyo kuona wamefanyiwa uhuni. Katika hili Mkono hana pa kuchomokea, sana sana anatakiwa kusimamia kwa makini utendaji wa bodi ilikuendelea kulinda heshima yake. Mikopo imekuwa haina maana, kwani mtu ameomba kukopa mathalani milioni 2, anachoenda kupewa laki 6 au 7, maana ya mkopo ikowapi? Tutafakari.

Nimesahihisha sehemu hiyo kama nilivyoshauliwa na Sam mwenyewe, hii ndiyo raha ya Blogu maana hapa tuna uhuru wa kubandika yale yauchomayo moyo: Makene
 
© boniphace Tarehe 10/21/2005 07:13:00 AM | Permalink |


Comments: 1


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved