Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Thursday, October 20, 2005
KIBONA ANIJIBU KUHUSU NILMUD MKONO
RAFIKI yangu Kibona ameandika makala yake nitayaweka hapa. Maoni yangu ya awali kuhusu Mbunge wa Musoma Vijijini na Mwenyekiti wa Bodi ya Makopo ya wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini Tanzania hayakumaanisha ufanisi wa Bodi hiyo.

Maoni yangu yalimlenga Mkono kutokana na ujasiri wa kukubali kumaliza mgomo wa wanafunzi UDSM kwa kwenda pale kuzungumza nao. Alisema yafuatayo, Mosi, Bodi yake ulicheleweshewa fedha na Wizara. Kumbuka Waziri wa wizara hiyo ndiye aliyempa ulaji hivyo kubaini uzembe wa wizara vyake ni jambo linaloitaji moyo na ujasiri. Pili, alipinga vipengele vya Fomu za mikopo na yeye kama mwanasheria kutamka kuwa havieleweki eleweki! Tatu akawataka wanafunzi kuandika kile wawezacho ili wasicheleweshewe fedha zao!

Hayo tu ndiyo yaliyokuwa maoni yangu kuhusu Mkono, kumbuka mwaka 2000 kulikuwa na mgomo mkubwa UDSM uliomtaka Sumaye kufika kuzungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania, aligoma! Kumbuka mgomo mwingine wa kitivo cha Uhandisi, kumbuka mgomo wa Masuala ya kufutwa mazoezi ya vitendo kwa wanafunzi wa Ualimu, kumbuka mgomo wa kupambana na vipengele vya Sheria ya Bodi ya Mikopo; yote hii ilifanyika na hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyejitokeza kuona umuhimu wa kutatua au kusikiliza kero za wanafunzi!

Bado kuna huyu mama Katibu wa Wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya Juu, nitamuandika wakati ukifika sasa namuweka kapuni. Huyu ni miongoni mwa akina mama wachache wanaokwamisha na kuchochea migomo na hana uwezo wa kupambana na matatizo ya elimu ya juu Tanzania. Sijui alipewaje kazi hiyo lakini si ni mtindo wa Tanzania wa kupeana madaraka kwa kujuana...

sasa endelea kumsoma Kibona hapa chini!

NIMEKUELEWA SANA MH MAKENE.NIMEJARIBU KUPITIA KASRI LAKO HAKIKA LINATISHA.LAKINI NOAMBA NIKUKOSOE KUHUSU MBUNGE WAKO NIMRODI MKONO AMBAYE KWA SASA NI MWENYEKITI WA BOARD YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU TANZANIA.NADHANI UNAJUA NI NINI KINAENDELEA MPAKA SASA KATIKA VYUO MBALIMBALI HAPA NCHINI.NGOGE NI ENDE MOJA KWA MOJA PALE MLIMANI AMBAPO NDIO NYUMBANI KWETU.

NI KAMA WIKI MBILI ZIMEPITA TANGU WASOMI WA HAPO MLIMANI WALIPOAMUA KUANDAMANA ILI KUMSHAWISHI NIMRODI NA BOARD YAKE KUSIKIA MATATIZO YA WATOTO WA WAKULIMA WALIOTOKA HUKO MIKOANI KUJA KUBUKUA HAPA MLIMANI NA HATIMAYE KUISHIA KWA NDUGU NA JAMAA MITAANI HAPA DAR BAADA YA BOARD KUTOA AHADI HEWA.

SWALI LINAKUJA,JE MKONO HAKULIONA HILO MPAKA APIGIWE KENGELE YA MAANDAMANO NA VITISHO VYA KUTOIPIGIA KURA CCM?.HAYA BAADA YA MANDAMANO NIMRODI WAKO BILA KUPENDA NA MIAVULI WAKE WAKAJA NKURUMAH KUWAELEZA UKWELI WANAFUNZI.

SWALI LA PILI KWA NINI UKWELI UNFICHWA HADI MAANDAMANO NDIPO MAMBO YANWEKWA WAZI?

MIMI NILITEGEMEA HIYO BOARD YA MIKOPO INGESHIRIKIANA NA UONGOZI WA VYUO KATIKA KUTATUA TAYIZO HILI, LAKINI KINACHOONEKANA SASA VYUO VINATAKA HELA WAKATI HUO HUO BOARD INA MKONO WA BIRIKA.MIMI NADHANI LAZIMA HIYO BOARD IKUBALI KUCHUKUA DHAMANA HIYO VINGINEVYO INAKUMBWA NA WIMBI LA MIGOMO KUTOKA VYUO VIKUU HASA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM AMBACHO KINAFUNDISHA WASIASA WENGI WENYE MLENGO WA KUSHOTO.PALE KUMEJAA VIPAJI HAKIFICHWI KITU MPAKA KIELEWEKE.

HAYA MLIMANI WAMEPEWA BOOM LAO BAADA YA MGOMO.WATOTO NAO WAMEFUATA NYAO ZA BABA KUDAI HAKI,MAANDAMO IFM,CBE, SUA,NA TUMAINI.

LAKINI NGOJE NIWACHAMBUA TUMAINI,KWANI LUNGU WALILOLISIMIKA SASA LIMEWAPIGA WENYEWE.BILA KUSAHAU MWAKAJANA MWEZI WA NNE NIKIWA PALE MLIMANI TULISHUSHIWA KIPIGO KIKALI NA NGUVU ZA DOLA BAADA YA KUPINGA BAADHI YAVIPENGELE KATIKA MSUADA HUO.TUMAINI UNIVERSITY AU MAARUFU ACADEMY WALUNGANA NA SERIKALI KUTUPONDA SISI WATOTO WA WAKULIMA TUNAOTEGEMEA MIKOPO.SASA WAO WANAANDAMA NINI?

LAKINI KWA UFUPI BWANA MAKENE IMEAONA DOSALI ILYOPO KATIKA BOARD HIYO.

VILE VILE NAWEZA KUSEMA KWAMBA HAKIKA WASOMI WA MLIMANI WANAONA MBALI.

KWA MAONO YANGU KWA SABABU WANAFUNZI BADO WANADHAMIRA KWAMBA KUPATA MKOPO NI HAKI YAO,BASI MGOMO UTAKAO FUATA NI MADAI YA KUONGEZEWA KIASI CHA FEDHA NA HILO HALINA UBISHI HII NI AGENDA ILIYOPO PALE MLIMANI UKIPITA SEHEMU MOJA INAYOITWA TBS MAARUFU KWA ULINGO WA SIASA.HAYA YETU MACHO.
 
© boniphace Tarehe 10/20/2005 11:38:00 AM | Permalink |


Comments: 0


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved