Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Tuesday, March 10, 2009
NIMESHINDWA KUTIMIZA AHADI
JUMAPILI iliyopita ilikuwa siku ya Wanawake Duniani. Siku hiyo ni muhimu sana kwangu na nilidhani kupitia eneo langu nizungumze machache. Akina mama hasa wa Afrika wanapitia vipindi vigumu mno katika maisha yao hasa sasa ambapo tabia za wanaume wengi kuanza kujiingiza katika tamaduni za magharibi.

Hali ya kuwathamini akina mama ambayo utamaduni wa Kiafrika ulikuwa ukifafanua sasa iko katika hatihati. Na akina mama nao wengi wameingia katika mtego wa kutotambua kuwa maisha yao ambayo ni ya muhimu sana katika dunia ynahitaji uvumilivu ambao wamezaliwa nao na kweli wanaumudu.

Nilijiwekea ahadi ya kuzindua kitabu katika siku hii; Kama wakumbuka chaitwa 'Barua kwa Mama' lakini bado sijafanikiwa kufanya hivi. Hata hivyo msomaji Barua kwa Mama ipo katika hatua njema; wakati ukifika itatoka. Binafsi siamini katika utunzi wa kukimbizana maana kazi za sanaa hazifi na ndio maana kila nisomapo muswada huu najikuta nacheka kwani unabeba kauli na maarifa ambayo yanaweza kuishi kwa miaka mingi zaidi. Salamu kwa akina mama wote.
 
© boniphace Tarehe 3/10/2009 03:18:00 AM | Permalink |


Comments: 1


   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved