Kasri, jumba la weledi waweza keti hapa na kupata ukitakacho. Chakula cha wakazi wa Kasri ni fikra na chakula hiki kimewapa thawabu wananchi wa nchi hii hali inayowafanya kutoziba midomo yao kila waonapo damu ya wanaonyanyaswa ikidondoka katika bahari ya dhiki, maangamizi na unyonyaji. Waweza nawe keti hapa na kula fikra hizi.
Friday, February 24, 2006
RAIS WA WATU
KAMA hujamtembelea ATHUMANI fanya hivyo mapema. Zipo picha amezificha kwenye Photo albamu na huko utaweza gundua mengi kama nilivyoweza kuipata hii hapa. Kwa mtazamo huu wa vipicha na vile vingine anavyotuonyesha Michuzi sasa hivi nadhani Tanzania ina rais wa watu, tumpe ushirikiano kwa kuwafichua wala rushwa na tutokomeze ufisadi kwa vitendo. Nasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko.
 
© boniphace Tarehe 2/24/2006 01:24:00 PM | Permalink |


Comments: 6


  • Tarehe 2/24/2006 1:55 PM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

    Kapiga simpo tu. kadet na sweta.Hiyo ndio T-shirt na jeans ya madingi. Wangekuwa wengine hapo suti mithili wanaingia mkutanoni UN.

    Walau nao wamasai wanywe maji ya viwandani leo. Lakini mwajua mzoea vya kunyonga vya kuchinja kwake vigumu. Isije kuwa hawa morani washazoea ya visimani na mitoni. Leo kupewa ya Mohamed Enterprises, Reginald Mengi na Bakhresa wataharisha hawa.

     
  • Tarehe 2/25/2006 1:10 AM, Mtoa Maoni: Blogger Reggy's

    nina wasiwasi, kama wataendelea kupata maji safi (mfano wa hayo kwenye chupa). au wataendelea kunywa maji kwenye visima pamoja na ng'ombe wao. Wanachotaka morani hawa ni suluhisho la kudumu, si maji ya dakika moja, kama vile JK yuko kwenye kampeni?

     
  • Tarehe 3/02/2006 1:27 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous

    ni kweli wapate vyanzo vya maji vya uhakika. kwa wakati huyo huo tumsaidie mzee ili ndoto na ahadi za kampeni zitimilizike! mark

     
  • Tarehe 3/04/2006 6:10 AM, Mtoa Maoni: Blogger FOSEWERD Initiatives

    hebu utuulizie kwa Athumani, huyo pembeni hapo ni Kapenjama? hii picha sijaikuta kule

     
  • Tarehe 3/04/2006 10:21 AM, Mtoa Maoni: Blogger John Mwaipopo

    Mark umenikumbusha Kapenjama UDSM.Alikuwa-ga machachari kweli kweli. lakini huyu hapa pembeni kama sio yeye vile. Kapenjama ana sura ya kizee zee hivi ingawaje ni kijana tu.

    Picha hii iko kwenye albamu ya Athumani. Angalia vizuri utaikuta.

     
  • Tarehe 3/18/2006 11:23 AM, Mtoa Maoni: Blogger FOSEWERD Initiatives

    Kweli yule bwana ni Machachari..na anaonekana ni machachari kweli....labda mzalendo pia...tulikutana Addis Ababa 2004, nikiwakilisha SA naye akiwakilisha TZ, alikuwa anajitambulisha "I am Kapenjama from the United Republic of Tanzania"....halafu unajua tena anaweka hizo r kwenye l...baada ya muda wote tukawa tunamuita United Repabric of Tanzania....he is a good guy!

     
   
 
Copyright 2006 © BONIPHACE MAKENE. All Rights Reserved